Jumatano, 13 Mei 2015

Kilimo cha papai!
Mjasiriamali mdogo kapitia mada mbalimbali mitandaoni, akafanya utafiti kidogo kwa kuongea na watu wawili watatu na kuangalia mipapai toka sehemu mbali mbali. Mjasiriamali akatembelea mashamba ya kawaida ambayo wakulima wamepanda mazao yao lakini wakiwa na miche michache ya papai. maendeo kama Kibaha, Shungubweni huko Mkuranga, Mbagala, Mbande mpaka Kimanzichana.

baada ya kujiridhisha kuwa kilimo cha papai kinawezekana mjasiramali mdogo akajinyanyua na kupambana katika kilimo cha papai.

Mbegu
Mjasisriamali akanunua mapapai makubwa ambayo angependa kuyapanda shambani kwake, akala papai na kuzitunza mbegu zake. Mbegu zikaanikwa vizuri hata zilipokauka zikawa tayari kupandwa kwenye kitalu.
Kitalu
Kitalu cha kawaida kabisa kikaandaliwa ndani ya uzio wa nyumba. Mjasiriamali akabeba udongo toka shambani kwake Kimanzichana hadi nyumbani kwake Kijichi. Huko akachanganya udongo na mbolea ya samadi na kisha kupakia kwenye vifuko. Vifuko vikapangwa vizuri na kumwagiliwa kwa zaidi ya wiki mbili; mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.



 

Baadaye mjasiriamali mdogo akapanda mbegu zake kwenye kitalu na kumwagilia asubuhi na jioni hadi miche ilipopendeza na kuwa tayari kupandwa shambani. Mjasiriamali hakuwa na utaalamu wa kuhesabu siku za miche kitaluni, bali alipoiangalia na kujiridhisha kuwa inafaa kupandwa; aliipakia kwa gari na kuipeleka shambani na kuipanda.


Miche shambani
Mjasiriamali akaendelea kuimwagilia miche ikiwa shambani, aliimwagilia asubuhi na jioni hata miche ikapendeza.


Changamoto
Mjasiriamali mdogo anasema changamoto kubwa ni mtaji wa kuendeshea kilimo. Kwamba kilimo kinahitaji mtaji wa kuendeshea shughuli za kilimo kama kulima, kupanda, kupalilia, kuweka mbolea na kutunza shamba kwa ujumla.
Bahati mbaya sana, hakuna benki iliyo tayari kumkopesha mjasiriamali huyu mdogo na hasa wakizingatia kuwa matunda ya ujasiriamali kama huu yanapatikana baada ya mwaka na zaidi. Hivyo basi mjasiriamali huyu mdogo ataendelea kuumia kwa mwaka mzima ili baadaye aanze kuvuna matunda ya jasho lake..

Mjasiriamali mdogo anaomba kwa wale walioguswa na juhudi zake na wanaofikiria kumsukuma katika mapambano hayo wawasiliane naye kwa namba 0787519910 ama kupitia huduma ya whatsapp.   


Maoni 0:

Chapisha Maoni

Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]

<< Nyumbani