Alhamisi, 14 Mei 2015

Karibu kwetu Kimanzichana

 Safari kwenda Kimanzichana
Sijui kuna uhusiano gani wa eneo hili na wimbo wa Sikinde ulioimbwa zamani sana ukisema "Aloo bwana, usiambiwe na watu ukifika Kimanzichana wewe utauwa uwa!!
Ni safari ya kilomita 80 kutoka stendi daladala ya Mbagala hadi kimanzichana. Ukielekea kusini mwa nchi yetu kupitia barabara maarufu ya Kilwa, utafika Mkuranga makao makuu ya wilaya kama km. 40-43 toka Mbagala na baadaye Kimanzichana. Ni astani wa mwendo wa saa moja kwa mwendo wa kawaida. Zipo daladala nyingi tu na muda wote zinazoanzia safari stendi ya daladala ya Mbagala hadi Kimanzichana ambapo nauli ni Tshs. 2,400/=.  

Getini Kimanzichana
Unapoingia Kimanzichana ukitokea kijiji kikubwa cha Mwarusembe kuna geti la maliasili na kituo maarufu kiitwacho Kimanzichana getini. Inakuchukua km. 2 toka hapo barabarani kuelekea kaskazini ambapo kuna kijiji kiitwacho Mkwechembe, ukipitia njia iendayo pwani. Njia hii ni maarufu na inapitika vipindi vyote vya masika na kiangazi.

Mazao yanayostawi
Mazao yanayolimwa na kustawi huko kwa uchache ni pamoja na Korosho kama zao la biashara, machungwa, nazi, mahindi, ufuta, kunde nk. Wenyeji pia wanafuga kuku ingawa ni kidogo kidogo kwa matumizi ya chakula na kwa nadra sana huuza mmoja mmoja ili kujipatia mahitaji muhimu.

Maji
Maji yanapatikana kwa kuchimba visima ama kwa kutumia mashine ama kwa kuchimba kienyeji. Vile vya kienyeji mchimbaji huchimba kwa jembe dogo na shima linakuwa na mduara mdogo tu, na mchimbaji anachimba kisima cha urefu wa futi zaidi ya 60. Uchimbaji huu ni hatari sana lakini wenyeji hawana wasiwasi nao na umesaidia sana upatikanaji wa maji.



Mashamba
Mashamba yanapatikana kwa bei nafuu, karibuni wale mupendao kuendeleza maneno ya kilimo kwanza...



Maoni 0:

Chapisha Maoni

Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]

<< Nyumbani