Jumapili, 24 Mei 2015

TUNDA PAPAI
Tunda papai tamu na lenye ladha ya mvuto.
Papai linastawi katika hali ya hewa ya kitropiki yenye joto kiasi, hali hii muafaka kabisa kwa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani na mingineyo yenye hali kama hiyo.

Udongo unaofaa kwa papai ni ule wenye rutuba na usiotuamisha maji. Endapo papai litapanwakwenye udongo unaotuamisha maji, mipapai haitadumu itadhurika na maji.

Mipapai ikipandwa na kuwekewa mbolea ya kutosha wastani wa kilo tano mpaka sita za samadi, upo uwezekano ikadumu kwa miaka mitatu ikitoa matunda. Mwaka wa kwanza wa kupandwa mazao huwa si mengi sana, lakini mwaka unaofuata mpapai huzaa sana na kadri miaka inayofuatia mpapa unapoteza uwezo wake wa kuzaa mapapai.



Inashauriwa kutunza mpapa kwa miaka mitatu na hapo kuing'o na kupanda mingine. Mipapai inaweza kupandwa na mazao mengine ambayo hayatauzidi urefu mpapai. Mazao yanayoweza kupandwa na mipapai ni pamoja na nanasi, mahindi nk.

Papai lina soko la uhakika. Papai likiwa shambani laweza kuuzwa kwa shilingi mia tatu 300/= mpaka mia tano 500/=. Hata hivyo papai likitoka shambani na likifikishwa barabarani hasa maeneo ya stendi za magari huko huko vijijini linauzwa siyo chini ya shilingi 1,000/= na likifikishwa mjini ni zaidi ya 1,500/= mpaka 2,000/= na zaidi kutegemea na ubora wake.

Mkulima makini mwenye heka moja aliyepanda mipapai kama 1,000 ana uhakika wa kupata wastani wa shilingi 300,000/= kwa wiki. na kama atakwenda zaidi na kupanda heka tatu basi ana uhakika wa kupata wastani wa shilingi 900,000/= kwa wiki

Mwandishi amefanya utafiti kidogo kwa wakulima wachache, ambao wamesema wanauza mapapai yao kwa walanguzi wadogo wadogo wapitao majumbani mwao kwa baiskeli. Walanguzi hao huwa na matenga makubwa na kununua papai moja kwa shilingi 100/= hadi 200/=. Hii inatokana na ukweli kwamba wanavijiji wengi huwa wamepanda miche michache mashambani mwao, aidha huwa inajiotea kutokana na kula mapapai na kutupa mbegu.

Ni maoni ya mwandishi wa makala hii kwamba hii nayo ni fursa inayoweza kumfanya mwananchi akapambana na maisha yake bila kusubiria ajira za serikali. Ikumbukwe kuwa mwanakijiji huyu pamoja na shughuli hii ya kilimo cha papai; anaweza kuwa na shughuli nyingine kama ya ufugaji wa kuku, mbuzi na ng'ombe wawili watatu wa maziwa.


Jumamosi, 16 Mei 2015

KIMANZICHANA JUMAMOSI YA LEO

Leo Jumamosi tumetembelea shamba letu; nyumbani kwetu Kimanzichana. Hali ya hewa ni nzuri wananchi walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kilimo kama kawaida. Mvua imekata kidogo kijua kinawaka fulani, hali ya mazao kwa wastani ni nzuri.

Wadau walioongozana hadi shambani wakafurahia kula matunda halisi na papo kwa hapo,tunda linatoka mtini linaliwa, muhugo unachimbwa shambani unaliwa, dafu linaanguliwa mtini linaliwa... shambani kuna raha yake bhana, asikwambie mtu!!





Alhamisi, 14 Mei 2015

SIKINDE NGOMA YA UKAE!!



Muziki wa Sikinde
Ninapenda sana muziki wa Sikinde; lakini pia napenda sana muziki wa OTTU... 
Kuna kipindi uliandaliwa mpambano wa bendi hizi mbili, huwaga napataga tabu sana. Hata hivyo nawapenda zaidi Sikinde. 
Hebu tupate ladha ya mashairi ya wimbo wao maarufu wa nawashukuru wazazi.

Wimbo una mashairi machache, lakini maudhuiyake ni mazito sana. Wimbo una fani iliyosheheniutamu wa hali ya juu.. Hongera sana Sikinde...

Nawashukuru wazazi…. Sikinde Ngoma ya Ukae!!
Nimeishi na wazazi wangu nikiwa bado mwanafunzi,
Sikuwahi kuishi peke yangu bila kuwa na wazazi wangu….!!

Baada ya kumaliza masomo nilipata kazi,
Wazazi wangu waliniusia jinsi ya kuishi na walimwengu…… X 2!!

Ya kuwa niwe na heshima kwa mkubwa na mdogo,
Hayo ndiyo mafanikio kwa maisha yangu ya baadaye !!

Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote, ushauri wao umeniletea mafanikio mema,
Sasa naishi na watu vizuri eeeh, sasa naishi na watu vizuri eeeeh..

Huku nilipo wazazi wangu sina ndugu, lakini kutokana na usia wenu wazazi wangu najiona kama nipo nyumbani eeeh mama!!

Karibu kwetu Kimanzichana

 Safari kwenda Kimanzichana
Sijui kuna uhusiano gani wa eneo hili na wimbo wa Sikinde ulioimbwa zamani sana ukisema "Aloo bwana, usiambiwe na watu ukifika Kimanzichana wewe utauwa uwa!!
Ni safari ya kilomita 80 kutoka stendi daladala ya Mbagala hadi kimanzichana. Ukielekea kusini mwa nchi yetu kupitia barabara maarufu ya Kilwa, utafika Mkuranga makao makuu ya wilaya kama km. 40-43 toka Mbagala na baadaye Kimanzichana. Ni astani wa mwendo wa saa moja kwa mwendo wa kawaida. Zipo daladala nyingi tu na muda wote zinazoanzia safari stendi ya daladala ya Mbagala hadi Kimanzichana ambapo nauli ni Tshs. 2,400/=.  

Getini Kimanzichana
Unapoingia Kimanzichana ukitokea kijiji kikubwa cha Mwarusembe kuna geti la maliasili na kituo maarufu kiitwacho Kimanzichana getini. Inakuchukua km. 2 toka hapo barabarani kuelekea kaskazini ambapo kuna kijiji kiitwacho Mkwechembe, ukipitia njia iendayo pwani. Njia hii ni maarufu na inapitika vipindi vyote vya masika na kiangazi.

Mazao yanayostawi
Mazao yanayolimwa na kustawi huko kwa uchache ni pamoja na Korosho kama zao la biashara, machungwa, nazi, mahindi, ufuta, kunde nk. Wenyeji pia wanafuga kuku ingawa ni kidogo kidogo kwa matumizi ya chakula na kwa nadra sana huuza mmoja mmoja ili kujipatia mahitaji muhimu.

Maji
Maji yanapatikana kwa kuchimba visima ama kwa kutumia mashine ama kwa kuchimba kienyeji. Vile vya kienyeji mchimbaji huchimba kwa jembe dogo na shima linakuwa na mduara mdogo tu, na mchimbaji anachimba kisima cha urefu wa futi zaidi ya 60. Uchimbaji huu ni hatari sana lakini wenyeji hawana wasiwasi nao na umesaidia sana upatikanaji wa maji.



Mashamba
Mashamba yanapatikana kwa bei nafuu, karibuni wale mupendao kuendeleza maneno ya kilimo kwanza...



KOCET 2014 RE-UNION

LONG LIVE KOCET...!!
KOCET RE UNION 2014
Waliokuwa wanachuo wa chuo cha ualimu Korogwe TTC; Machi 2015 walikutana kwa party ya get together.
Ni utamaduni wa wanachuo hao kukutana kila mwaka kwa party na kubadilishana mawazo na kujipangia mikakati mbalimbali kwa faida ya chuo chao.

Wanachuo hao walikutana katika club ya Calabash iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa wanachuo waliohudhuria ni Mohamed Rajabu Tengerusa, Edward Emmanuel, Maria Mbotto, Julius Frank, Hajira Mmambe, Erick Shartiel Mturuki, Hilda Arch, Kaleb, Michael Onesmo OJ, Verediana Kajala VDK, Agatha, Hasan Dassi na wengineo wengi.

watu walikunywa, wakala,wakacheza muziki, wakabadilishana mawazo, wakakumbuka amisha ya chuo miaka ileee... hakika ilipendeza. 





Mwaka 2013 Re Union kama hiyo ilifanyika pale Landmark Hotel mitaa ya Ubungo. Hii ilihudhuriwa na watu wachache kama wanavyoonekana hapo chini pichani....




Mwaka 2012 ilifanyika tena pale Landmark hotel na ilikuwa kama hivi












Jumatano, 13 Mei 2015

Kilimo cha papai!
Mjasiriamali mdogo kapitia mada mbalimbali mitandaoni, akafanya utafiti kidogo kwa kuongea na watu wawili watatu na kuangalia mipapai toka sehemu mbali mbali. Mjasiriamali akatembelea mashamba ya kawaida ambayo wakulima wamepanda mazao yao lakini wakiwa na miche michache ya papai. maendeo kama Kibaha, Shungubweni huko Mkuranga, Mbagala, Mbande mpaka Kimanzichana.

baada ya kujiridhisha kuwa kilimo cha papai kinawezekana mjasiramali mdogo akajinyanyua na kupambana katika kilimo cha papai.

Mbegu
Mjasisriamali akanunua mapapai makubwa ambayo angependa kuyapanda shambani kwake, akala papai na kuzitunza mbegu zake. Mbegu zikaanikwa vizuri hata zilipokauka zikawa tayari kupandwa kwenye kitalu.
Kitalu
Kitalu cha kawaida kabisa kikaandaliwa ndani ya uzio wa nyumba. Mjasiriamali akabeba udongo toka shambani kwake Kimanzichana hadi nyumbani kwake Kijichi. Huko akachanganya udongo na mbolea ya samadi na kisha kupakia kwenye vifuko. Vifuko vikapangwa vizuri na kumwagiliwa kwa zaidi ya wiki mbili; mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.



 

Baadaye mjasiriamali mdogo akapanda mbegu zake kwenye kitalu na kumwagilia asubuhi na jioni hadi miche ilipopendeza na kuwa tayari kupandwa shambani. Mjasiriamali hakuwa na utaalamu wa kuhesabu siku za miche kitaluni, bali alipoiangalia na kujiridhisha kuwa inafaa kupandwa; aliipakia kwa gari na kuipeleka shambani na kuipanda.


Miche shambani
Mjasiriamali akaendelea kuimwagilia miche ikiwa shambani, aliimwagilia asubuhi na jioni hata miche ikapendeza.


Changamoto
Mjasiriamali mdogo anasema changamoto kubwa ni mtaji wa kuendeshea kilimo. Kwamba kilimo kinahitaji mtaji wa kuendeshea shughuli za kilimo kama kulima, kupanda, kupalilia, kuweka mbolea na kutunza shamba kwa ujumla.
Bahati mbaya sana, hakuna benki iliyo tayari kumkopesha mjasiriamali huyu mdogo na hasa wakizingatia kuwa matunda ya ujasiriamali kama huu yanapatikana baada ya mwaka na zaidi. Hivyo basi mjasiriamali huyu mdogo ataendelea kuumia kwa mwaka mzima ili baadaye aanze kuvuna matunda ya jasho lake..

Mjasiriamali mdogo anaomba kwa wale walioguswa na juhudi zake na wanaofikiria kumsukuma katika mapambano hayo wawasiliane naye kwa namba 0787519910 ama kupitia huduma ya whatsapp.   


Jambo KOCET.....



Wapendwa wana KOCET!
Nina furaha kuwafahamisha kuwa nimeanzisha blog ambayo ninaamini pamoja na habari nyingine lakini pia itajikita sana katika kujadili mambo ya kijamii kwa manufaa yetu kwa ujumla.

Nimeanza na post hii yenye picha na habari za Chuo cha ualimu Korogwe ama tulikiita KOCET.

Chuo cha ualimu Korogwe kipo wilaya Korogwe kilomita chache kutoka stendi kuu ya mabasi ya Korogwe. Chuo hicho miaka ya 1990 hadi 1993 kilikuwa kikitoa mafunzo kwa walimu wa Diploma ya ualimu na daraja A.

Miye nilikuwepo chuoni hapo miaka ya 1990 hadi 1993 nilipomaliza Diploma yangu ya ualimu.

Tumekuwa tukijadiliana sana katika mitandao ya whatsapp na facebook, ni imani yangu hapa pia tutajadili na kufanya mambo makubwa kwa kadri tutakavyojaaliwa. Kupitia blog hii tutawapongezana kwa tuyuu, harusi, vyeo, elimu nk lakini pia tutapata habari nyinginezo zinazofanana na hizo.. 

Lakini pia tutajadili mambo ya kijamii, kiuchumi, saikolojia na mengineyo ambayo sisi tuna uzoefu nayo. Nachelea kujadili mambo ya kisiasa kwa sababu ya tofauti za kisiasa, mitizamo na kiitikadi nk.

Karibuni sana.....

CHUO CHA UALIMU KOROGWE [KOCET]

Chuo cha Ualimu Korogwe [KOCET]
Chuo hiki kipo kilomita chache kutoka stendi kuu ya mabasi wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga. Chuo kwenye miaka ya 1990 hadi 19993 kilikuwa kinatoa mafunzo ya ualimu wa ngazi ya Diploma na cheti daraja A.
Pia kulikuwa kinatoa mafunzo kwa walimu waliokuwa wakibadili madaraja ya ualimu Daraja C kwenda A wakiitwa in-service.
Nilibahatika kusoma ualimu daraja la Diploma miaka mitatu na nilihitimu mwaka 1993.

Ninawakumbuka sana walimu wangu akiwemo mkuu wa chuo Mwl. Sylivester Mgoma, makamu mkuu wa chuo Mwl. Masawe, mwadili wa wanachuo Mwl. Gahu [RIP], Mwl. Mtoahanje, Mwl. Alex kocha wa mpira, Mwl. Muyombo, Mwl. Kipesha, Mwl. Mjema....
Lakini kulikuwa na watu maarufu kama mpishi mmoja akiitwa mgosi Hassani...
Hakika maisha ya KOCET yalikuwa matamusana. Nitatupiamo baadhi ya picha za KOCET miaka hiyoo.
 Picha ya muonekano kama unaingia chuoni

 Mitaa ya jengo la utawala miaka ya 1990